Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

UNDP inasaidia kuhakikisha watu zaidi ya milioni moja wanapata maji salama Iraq

UNDP inasaidia kuhakikisha watu zaidi ya milioni moja wanapata maji salama Iraq

Shirika la Umoja wa Mataifa la Mpango wa Maendeleo(UNDP) na jimbo la Sulaimaniyah nchini Iraq wametia saini makubaliano ya kukarabati mfumo wa maji jimboni humo . Assumpta Massoi na habari kamili.

(TAARIFA YA ASSUMPTA)

Kwa mujibu wa mwakilishi wa UNDP , na mtratibu mkazi wa Umoja wa Mataifa Iraq Bi Lise Grande, jimbo na watu wa Sulaimaniyah wamewakaribisha na kuwasaidia wakimbizi wa ndani na familia za wakimbizi.

Miundombinu ya mji iko katika shinikizo kubwa kwa sababu watu wengi wanahitaji huduma, na tunafurahi kwamba tunaweza kusaidiajimbo hili kwa kukatrabati mfumo muhimu wa maji ameongeza Bi Grande.

Kwa ufadhili kutoka Japan ,UNDP na jimbo la Sulaimaniyah , ukarabati wa mfumo huo wa maji utaanza mara moja ,na kuwanufaisha ya maji salama ya kunywa watu zaidi ya milioni 1.1 wengi wakiwa ni wakimbizi na wakimbizi wa ndani.