Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Benki ya dunia yawezesha Drones kupiga picha angani Tanzania

Benki ya dunia yawezesha Drones kupiga picha angani Tanzania

Nchini Tanzania benki ya dunia imesaidia mradi wa kupiga picha angani kwa kutumia ndege zisizo na rubani au Drones, kwa lengo la kufanikisha mradi wa umilikishaji ardhi kwa watu zaidi ya Laki Tatu.

Kwa kushirikiana na wadau Tume ya Sayansi na Teknolojia, COSTECH , Wizara ya ardhi, na Uhurulabs mradi huo unalenga kusaka suluhu za kukabiliana na mafuriko pamoja na migogoro baina ya wakulima na ardhi kama anavyoelezea mmoja wa wakulima Severina Mwangeru.

(Sauti ya Severina)

Wizara ya ardhi nchini humo inasema mara ya mwisho picha za ardhi kutoka angani zilipigwa mwaka 2008 na hivyo mradi ni muhimu kama anavyosema Severina.

(Sautiya Severina)