Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Wataalamu wa UM watiwa hofu na taarifa za ghasia dhidi ya wanasheria Burundi

Wataalamu wa UM watiwa hofu na taarifa za ghasia dhidi ya wanasheria Burundi

Kamati ya Umoja wa Mataifa dhidi ya utesaji imeelezea wasiwasi mkubwa kufuatia ripoti za ghasia na uonevu dhidi ya wanasheria wanne nchini Burundi, waliotoa taarifa kwa kamati hiyo wakati wa tathimini maalumu ya Burundi mjini Geneva. Amina Hassan na taarifa kamili.

(TAARIFA YA AMINA)

Kamati hiyo imetuma barua kwa balozi wa Burundi kwenye Umoja wa Mataifa ikitaka hakikisho la haraka kwamba hakuna mtu yeyote wa asasi za kiraia Burundi atakayeadhibiwa kwa kutoa ushirikiano kwa kamati hiyo.

Wanasheria hao wanne Armel Niyongere, Lambert Nigarura, Dieudonné Bashirahishize naVital Nshimirimana walichangia ripoti mbadala kwenye kamati hiyo kutoka kwa muungano wa mashirika yasiyo ya kiserikali, na watatu walihudhuria kikao cha tathimini mjini Geneva Julai 28 na 29.

Na 29 Julai mwendesha mashitaka mkuu wa serikali aliagizwa kuwaengua wanasheria hao kwenye baraza la wanataaluma wa sheria kwa madai kwamba wamejihusisha na makosa kadhaa ikiwemo jaribio la mapinduzi.