Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Unyonyeshaji mtoto uanze saa moja tu baada ya mtoto kuzaliwa

Unyonyeshaji mtoto uanze saa moja tu baada ya mtoto kuzaliwa

Tarehe Mosi hadi Saba Agosti ya kila mwaka ni wiki ya Unyonyeshaji, siku ambayo Umoja wa Mataifa imetenga kuangazia jambo hili adhimu kwa makuzi ya mtoto na kwa mustakhbali wake wa baadaye. Shirika la afya duniani, WHO linasema kila mama mzazi anaweza kunyonyesha, alimradi apatiwe taarifa sahihi na jamii nayo imuunge mkono, sanjari na mfumo wa afya. Colostrum, ambayo ni maziwa yenye rangi ya manjano na mazito yatokayo pindi tu mama anapojifungua, yanaelezwa na WHO kuwa ni muhimu sana kwa mtoto aliyezaliwa na mama anapaswa kuanza kunyonyesha saa moja tu baada ya kujifungua. Na mtoto anatakiwa apatiwe maziwa ya mama bila kitu kingine chochote kwa miezi sita na baada ya hapo maziwa ya mama yaendelee na vyakula vingine hadi miaka miwili na kuendelea. Je Afrika Mashariki hali ikoje? Tuanzie Kagera nchini Tanzania, kwake Tumaini Anatory wa Radio Washirika Karagwe FM na hatimaye kwake Ramadhani Kibuga mwandishi wetu wa Maziwa Makuu kutoka mji  mkuu wa Burundi, Bujumbura.