Ban ashiriki kuubeba mwenge wa Olimpiki, kabla ya kuanza Rio2016

Ban ashiriki kuubeba mwenge wa Olimpiki, kabla ya kuanza Rio2016

Tuanze na Olimpiki, ambapo Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, Ban Ki-moon, yupo jijini Rio, Brazil, ambako leo anashiriki shughuli zinazohusiana na michezo ya Olimpiki ya Rio2016. Amina Hassan na maelezo zaidi.

Taarifa ya Amina

Kwanza kabisa, Ban ameshiriki katika kuubeba mwenge wa Olimpiki, akiwa na Rais wa Kamati ya Kimataifa ya Olimpiki, Thomas Bach.

Nats

Katibu Mkuu anatarajiwa pia kufanya mazungumzo na Meya wa Rio de Janeiro, Eduardo da Costa Paes.

Baadaye jioni, Ban atahudhuria hafla ya ufunguzi wa michezo ya Olimpiki ya 31, katika uwanja wa  Olimpiki wa Maracanã.