Skip to main content

UNICEF inakabiliana na mtafaruku wa lishe Sudan Kusini

UNICEF inakabiliana na mtafaruku wa lishe Sudan Kusini

Nchini Sudan Kusini , Shirika la Umoja wa Mataifa la Kuhudumia Watoto(UNICEF) na washirika wake , wanakabiliana na tatizo la ongezeko ukosefu wa uhakika wa chakula jambo ambalo linaathiri pakubwa watoto mijini na vijijini . John Kibego na ripoti kamili.

(Taarifa ya Kibego)

Tangu mwanzo wa mwaka huu UNICEF inasema imeshatibu watoto 120,000 wenye umri wa chini ya miaka mitano walioathirika vibaya na utapiamlo.

Hilo ni ongezeko la asiliomia 50 ikilinganishwa na mwaka jana na ni asilimia 150 ikilinganishwa na mwaka 2014.

Kwa mwaka huu shirika hilo limeweka lengo la kuwatibu watoto 166,000 , lakini kutokana na ongezeko la mahitaji idadi mpya ni zaidi ya watoto 250,000. Christophe Boulierac ni msemaji wa UNICEF.

(SAUTI YA BOULIERAC)

"Moja ya sababu za kuongezeka kwa kesi hizi ni kuongezeka kwa kiwango cha mfumuko wa bei ambayo imesababisha  umesababisha matumizi ya msingi kuwa magumu,mapigano yanayoendela pia yanasabisha ugumu kwetu kutoa msaada , barabara nyingi hazipitiki kwa sababu ya mapigano".