Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Zeid alaani unyongaji wa watu wengi Iran

Zeid alaani unyongaji wa watu wengi Iran

Kamishina Mkuu wa haki za binadamu wa Umoja wa mataifa Zeid Ra’ad Al Hussein Ijumaa amelaani vikali unyongaji wa watu 20 uliofanyika wiki hii nchini Iran kwa madai ya kuhusika na makossa ya ugaidi.

Duru zinasema karibu watu wote walionyiongwa ni kutoka kundi la Wasuni walio wachache katika jamii ya Wakurdi.

Ofisi ya haki za binadamu ya Umoja wa mataifa imesema katika kesi nyingi kumekuwa na shaka ya kutendeka haki, kuheshimiwa mchakato mzima wa kesi na haki za watuhumiwa. Zeid amesema huo ni ukkukwaji mkubwa wa haki.

Pia amelaani unyongaji uliofanyika mwezi uliopita wa mvulana wa miaka 19 Hassan Afshar, ambaye alikuwa na umri wa miaka 17 tu alipokamatwa na kuhukumiwa kwa kosa la ubakaji.