Skip to main content

Mlipuko wa Hepatitis E watangazwa Darfur, Sudan

Mlipuko wa Hepatitis E watangazwa Darfur, Sudan

Ofisi ya Umoja wa Mataifa inayoratibu masuala ya kibinadamu, OCHA, imesema kuwa mlipuko wa homa ya ini aina ya hepatitis E umetangazwa kule Sortony, Darfur Kaskazini, nchini Sudan,  ambapo watu 134 wana dalili za homa hiyo.

Kwa mujibu wa taarifa ya OCHA, msimu wa sasa wa mvua huenda ukachangia  uchafuzi wa mazingira kwa sababu ya vyoo kufurika, na kwamba mlipuko huo huenda ukaendelea iwaopo suala la msongamano wa watu waliolazimika kuhama makwao halitashughulikiwa.

Wadau wa kibinadamu wa huduma za afya, maji, na kujisafi, wanashirikiana na Wizara ya Afya nchini Sudan kukabiliana na visa vya kuharisha.

Takriban watu 80,000 wameathiriwa na mvua nzito na mafuriko nchini Sudan mwaka huu 2016.