Nchi za Amerika ya Kaskazini na Kati zaahidi kuwalinda wakimbizi

4 Agosti 2016

Shirika la Umoja wa mataifa la kuhudumia wakimbizi UNHCR , limekaribisha tamko la  San Jose la kuchukua hatua lililotolewa leo, ambapo nchi tisa za Amerika Kaskazini na Kati zimeahidi kuwalinda wakimbizi. Joshua Mmali na taarifa kamili.

(TAARIFA YA JOSHUA MMALI)

Tamko hilo la pamoja ni la kuhakikisha ulinzi kwa wakimbizi kutoka Amerika ya Kati  ni hatua kubwa kabla ya mkutano wa Umoja wa Mataifa na Marekani kuhusu wakimbizi na wahamiaji mwezi ujao wa Septemba.

Kamishima mkuu wa wakimbizi Filippo Grandi amesema inaridhisha na kutia moyo sana kuona nchi za Amerika zinakuja pamoja na msimamo wa kikanda wa kubuni suluhisho shirikishi kwa ajili ya watu wanaohitaji msaada wa kuokoa maisha.

Katika taarifa hiyo  serikali za Belize, Canada, Costa Rica, El Salvador, Guatemala, Honduras, Mexico, Panama na Marekani,  zimeafiki  kwamba kuna haja ya kuwalinda kikanda waomba hifadhi, wakimbizi na wakimbizi wa ndani.

 

♦ Kurambaza ukurasa mahsusi wa Siku ya Kiswahili Duniani bofya  hapa.
♦ Iwapo ungependa kupokea taarifa kutoka UN News Kiswahili kila wakati zinapochapishwa jisajili  hapa.
♦ Pia unaweza kupakua apu ili kusikiliza matangazo yetu wakati wowote popote ulipo.
♦ Tembelea pia chaneli yetu ya Youtube na pia Soundcloud na Twitter