Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Tunaendelea na uchunguzi wetu Syria kuhusu kemikali- OPCW

Tunaendelea na uchunguzi wetu Syria kuhusu kemikali- OPCW

Shirika la kupinga matumizi ya silaha za kemikali, OPCW, linaendelea kuchunguza ripoti za hivi karibuni kutoka vyombo vya habari zinazodai kuwa silaha za memikali zimetumika wakati wa mashambulizi nchini Syria.

Mkurugenzi Mkuu wa OPCW Ahmet Üzümcü amesema ripoti hizo zinatia wasiwasi mkubwa na hivyo uchunguzi unaofanyika unajikita kwenye taarifa za kuaminika inazopokea ikiwemo kutoka nchi wanachama wa mkataba wa kimataifa wa kuzuia silaha za kemikali.

Bwana Üzümcü amesema nchi hizo wanachama zinaamini kuwa matumizi yoyote ya silaha za kemikali yanayofanywa na mtu yoyote katika mazingira yoyote ni jambo baya ambalo pia ni kinyume na maadili yaliyowekwa na jamii ya kimataifa.