Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Timu ya Olimpiki ya wakimbizi yakaribishwa rasmi Brazil:

Timu ya Olimpiki ya wakimbizi yakaribishwa rasmi Brazil:

Timu ya Olimpiki ya wanamichezo wakimbizi imekaribishwa rasmi mjini Rio de Janeiro Brazili tayari kwa mashindano.

Kwa mujibu wa shirika la Umoja wa mataifa la kuhudumia wakimbizi UNHCR, Wanamichezo hao watakaowakilisha wakimbizi milioni 60 duniani wamekaribishwa rasmi na wajumbe wa kamati ya kimataifa ya Olimpiki IOC, akiwemo Rais wa IOC Thomas Bach.

(SAUTI THOMAS)

“Huu ni mwanzo wa safari, kwa sababu baada ya michezo ya Olimpiki kufungwa bila shaka tutaendelea kuwasaidia wanamichezo wakimbizi wa Olimpiki na tutawasaidia katika michezo na katika maisha,”

Naye mmoja wa wanamichezo hao, Biel Pur mkimbizi kutoka Sudan Kusini ambaye hajua hata wapi waliko wazazi wake kutokana na mchafuko yanayoendelea, amesema..

(SAUTI YA PUR)

Hatuna wazazi au ndugu katika maisha yetu, lakini sasasisi ni mali ya jamii, tunajihisi sasa ni binadamu, kuwa na hisia za ubinadamu”

Michuano ya Olimpiki inafunguliwa rasmi kesho Ijumaa Julai 5.