Tunachukua hatua kurahisisha utumiaji fedha kutoka ughaibuni- Rwanda

Tunachukua hatua kurahisisha utumiaji fedha kutoka ughaibuni- Rwanda

Serikali ya Rwanda imeanza kuchukua hatua kuhakikisha inapata vyanzo mbadala vya kufadhili maendeleo endelevu hususan kupitia mapato yatokanayo na fedha zinazotumwa na raia wake wanaoishi ughaibuni, badala ya kutegemea mikopo kutoka nje pekee.

Hatua hizo ni sehemu ya mapendekezo ya ripoti ya Kamati ya biashara na maendeleo ya Umoja wa Mataifa, UNCTAD iliyozinduliwa mjini Nairobi, Kenya mwezi uliopita kama anavyoelezea mchumi mkuu katika Wizara ya Fedha ya Rwanda Leonard Rugwabiza.

(Sauti ya Leonard)

Bwana Rugwabiza ambaye alihojiwa kando ya mjadala wa ripoti hiyo ya UNCTAD mjini Kigali, Rwanda, amesema idadi ya wanyarwanda walioko ughaibuni ni ndogo lakini..

(Sauti ya Leonard)

UNCTAD inasema zaidi ya dola Bilioni 600 zinahitajika kila mwaka hadi ifikapo mwaka 2030 ili kufanikisha malengo ya maendeleo endelevu na hilo linawezekana iwapo nchi zitategemea zaidi vyanzo vya ndani vya mapato badala ya mikopo na misaada ya maendeleo.