Skip to main content

ISIS inaendelea kutekeleza mauaji ya kimbari dhidi ya Wayazidi- Ripoti

ISIS inaendelea kutekeleza mauaji ya kimbari dhidi ya Wayazidi- Ripoti

Ikiwa leo ni miaka miwili tangu shambulizi la kikatili la ISIS dhidi ya Wayazidi nchini Syria, Kamisheni huru ya kimataifa kuhusu Syria imesema kuwa kikundi hicho cha kigaidi bado kinatekeleza uhalifu uliotekelezwa mnamo Agosti Tatu 2014 dhidi ya Wayazidi, yakiwemo mauaji ya kimbari.

Awali mnamo tarehe 16 Juni, 2016, Kamisheni hiyo ilitoa ripoti iliyobainisha uhalifu uliotendwa na ISIS dhidi ya Wayazidi katika mkoa wa Sinjar nchini Syria, ukiwemo mauaji ya kimbari, uhalifu dhidi ya ubinadamu, na uhalifu wa kivita.

Kamisheni imesema, bado wanawake na watoto zaidi ya 3,200 wanashikiliwa mateka na ISIS, wakitendewa ukatili wa aina zote.

Wengi wao wapo nchini Syria, ambako wanawake na wasichana wa Kiyazidi bado wanatumikishwa kama watumwa wa kingono, huku wavulana wakifundishwa itikadi kali na kutumikishwa katika vita.