Skip to main content

Ni muhimu kutumia tekinolojia na ramani kubaini maeneo yaliyoathirika na njaa:WFP

Ni muhimu kutumia tekinolojia na ramani kubaini maeneo yaliyoathirika na njaa:WFP

Shirika la mpango wa chakula duniani WFP limesema ni muhimu kutumia teknolojia na ramani ili kubaini maeneo yaliyoathirika na ukame na kuweza kuyasaidia. Brian Lehander na habari kamili

(TAARIFA YA BRIAN )

Katika kampeni maalumu ya kutokomeza njaa shirika hilo linasema maeneo mengi ya Kusini mwa Afrika yameathirika na ukame uliochangiwa pakubwa na El nino na kusababisha mamilioni ya watu kuhitaji haraka msaada wa chakula, kilimo na mahitaji mengine muhimu.

WFP imetaja miongoni mwa nchi zilizoathiorika zaidi kuwa ni Msumbiji, Angola na Malawi na Ili kuwasaidia kwa wakati watu wanaohitaji msaada shirika hilo inatumia teknolojia kupata picha halisi ya hali ya chakula kama anavyofafanua mkuu wa masuala ya kiuchumi wa WFP Arif Husain

(SAUTI YA ARIF HUSAIN)

"Kazi yetu ni kuhakikisha kwamba tunatakwimu sahihi kuhusu waathirika, wanapoishi, sababu gani zimewafanya kuhitaji msaada , na kwa muda gani na ni msaada gani utakuwa bora zaidi kuwasaidia".