Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Balozi mwemwa wa UNICEF McGregor ashuhudia madhila kwa watoto Iraq

Balozi mwemwa wa UNICEF McGregor ashuhudia madhila kwa watoto Iraq

Balozi mwema wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Kuhudumia Watoto(UNICEF) Ewan McGregor amezuru Kaskazini mwa Iraq juma lililopita , kushuhudia jinsi vita nchini Iraq na Syria vilivyoathiri maisha ya watoto.

Maelfu ya watoto wameuawa , kujeruhiwa, kutenganishwa na wazazi wao, kushinikizwa kufanya kazi, kuteswa na kuingizwa kwenye vita vya silaha.

Wakati wa ziara yake McGregor ametembelea kambi ya Debaga na kukutana na familia zilizokimbia vita mjini Mosoul na viunga vyake , pia ametumia muda wake kuketi na wakimbizi wa Syria na familia za wakimbizi wa ndani Iraq katika kambi mbalimbali na jamii za karibu na Erbil.

Kwa mujibu wa UNICEF hali ya watoto inazidi kuwa mbaya Iraq , ambapo watoto milioni 3.6 ikiwa ni mtoto mmoja kati ya watano wako katika hatari ya kufa, kujerihiwa, kufanyiwa ukatili wa ngono, kutekwa na kuingizwa jeshini na makundi yenye silaha.