Idadi ya vifo vya wahamiaji yaongezeka :IOM

Idadi ya vifo vya wahamiaji yaongezeka :IOM

Shirika la Kimataifa la Uhamiaji(IOM) limesema hadi sasa zaidi ya wahamiaji 4,000 wamefariki dunia ikiwa ni ongezeko la zaidi ya wahamiaji 1000 kwa mwaka huu ikilinganishwa na mwaka jana.

Taarifa ya IOM imenukuu ripoti ya mradi wa wahamiaji waliotoweka wa shirika hilo, imesema mwaka jana wakati huu, wahamiaji zaidi ya takribani 3,000 walifariki hiyo ikiwa ni ongezekao la asilimia 26 ikilinganishwa na miezi saba ya mwanzo ya mwaka 2015.

Mwaka 2014 katika kipindi cha meizi saba ya mwanzo jumla ya zadi ya wahamiaji 2,000 walifariki.

IOM inasema katika bahari ya Mediterranean mwaka huu idadi yavifo imefikia zaidi ya 3,000 ambapo IOM nchini Libya imeripoti kuonekana kwa miili 120 katika pwani ya Sabratha mwezi uliopita.