Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Hali ni mbaya Sudan Kusini msaada na ulinzi vyahitajika: O’Brien

Hali ni mbaya Sudan Kusini msaada na ulinzi vyahitajika: O’Brien

Mratibu na Mkuu wa Masuala ya Kibinadamu wa Umoja wa Mataifa, Stephen O’Brien amesema Sudan Kusini iko katika hali mbaya, na inahitaji msaada na ulinzi kwa maelfu ya watu waliotawanywa na machafuko.

O’Brien ambaye yuko katika ziara ya siku tatu nchini humo tangu Agosti Mosi, ameyasema hayo baada ya kuzuru Juba na eneo la Wau ambako athari ni kubwa zaidi.

Amesema watu wanahitaji huduma za chakula, maji, afya na hata elimu. Ameshuhudia maelfu wakiendelea kukimbilia nchi jirani na pia kusikia adha zinazowakabili waathirika hivyo akasisitiza..

(SAUTI YA O’BRIEN)

“Hali ni mbaya sana hivyo ambacho lazima tufanye ni kuhakikisha huduma zinatolewa na usalama unapatikana , ndio maana tunajikita na ulinzi wa raia lakini pia kuwapa huduma wanazohitaji kuokoa maisha ili kuhakikisha wanaweza kuangalia watoto wao, wanapata huduma za afya na elimu.”