Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Nchi zilinde taswira zao kwa kulinda watoto: Ban

Nchi zilinde taswira zao kwa kulinda watoto: Ban

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki Moon amezitaka nchi wanachama kulinda  taswira zao kwa kulinda haki za watoto katika mataifa yao. Joseph Msami  na taarifa kamili.

(TAARIFA YA MSAMI)

Akongea wakati wa mjadala wa wazi wa baraza la usalaam la Umoja wa Mataifa kuhusu watoto katika maeneo ya vita Ban amesema lengo la Umoja wa Mataifa ni kulinda watoto dhidi ya hatari na kwamba usalama wa dunia unazidi kuzorota na kuathiri zaidi watoto.

Kadhalika Katibu Mkuu amesema zipo sheria zinazotumika vitani mojawapo ikiwa ni kulinda  hospitali na shule pamoja na watoto kutojumuishwa vitani.

Kwa upande wake msaidizi  wa Katibu Mkuu kuhusu watoto maeneo ya vita Leila Zerrougui amesema ripoti kuhusu hali ya watoto vitani inatisha kwani watoto wanazidi kupitia madhila kadhaa katika sehemu za vita na akatolea  mfano wa madhila kwa watoto barani Afrika.

( SAUTI ZERROUGUI)

‘‘Majuma mawili tu yaliyopita nchini Somalia, nilishuhudia wavulana wakihukumiwa kifo kwa tuhuma za kujihusisha na kundi la kigaidi la Al shabaab.  Hili halikubaliki kama matokeo ya wa watoto wanaponusuriwa katika makundi yenye silaha.’’