Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

UNRWA yasaidia wakimbizi kulipa kodi ya nyumba, ukarabati

UNRWA yasaidia wakimbizi kulipa kodi ya nyumba, ukarabati

Shirika la Umoja wa Mataifa linalowasaidia wakimbizi wa Kipalestina (UNRWA), limesema kuwa limeweza kutoa dola milioni 2.5 kwa ajili ya kuwasaidia wakimbizi wa Kipalestina kulipa kodi ya nyumba na ukarabati wa miundombinu yao.

Fedha hizo zitasaidia familia 659 za wakimbizi katika Ukanda wa Gaza, ambao wataanza kupokea usaidizi huo wiki hii.

Taarifa ya UNRWA imesema kuwa makazi ya dharura, yakiwemo ukarabati wa nyumba na ujenzi mpya ni suala la kipaumbele kwake.

Kwa mantiki hiyo, UNRWA imeeleza dhamira yake kuendelea kuzisaidia familia zilizoathiriwa, lakini inahitaji ufadhili mpya ili iweze kuendeleza programu yake ya usaidizi wa kifedha.