JMEC yahimiza uhuru wa kutembea, na sitisho la mapigano liheshimiwe Sudan Kusini

1 Agosti 2016

Kamisheni ya pamoja ya kufuatilia na kutathmini hali nchini Sudan Kusini (JMEC), imeeleza wasiwasi wake kuhusu hali iliyopo sasa nchini humo.

Hii ni kufuatia mkutano wake wa ngazi ya juu uliofanyika mjini Khartoum, Sudan, mnamo Jumapili ya Julai 31, 2016.

Katika taarifa, kamisheni hiyo imelaani mapigano ya hivi karibuni kati ya SPLA-IG na SPLA-IO, na kutaka uwepo uhuru wa watu kutembea, pamoja na kufanyika uchunguzi ili kuwe na uwajibikaji kwa ukiukwaji wa sitisho la mapigano.

Taarifa hiyo ya JMEC pia imesema kuwa operesheni zinazowalenga viongozi wa upinzani zina hatari ya kuchochea ghasia kwa kiwango kikubwa, na kutaka operesheni hizo zikomeshwe mara moja.

 

♦ Tafadhali iwapo unataka kupokea taarifa kutoka UN News Kiswahili kila wakati zinapochapishwa jisajili  hapa.
♦ Pia unaweza kupakua apu ili kusikiliza matangazo yetu wakati wowote popote ulipo.
♦ Tembelea pia chaneli yetu ya Youtube na pia Soundcloud