Tunakabiliana na ukatili wa kingono na kijinsia Sudan Kusini: UNMISS

1 Agosti 2016

Ujumbe wa Umoja wa Mataifa nchini Sudan Kusini UNMISS umeongeza doria na ulinzi kwenye kambi za raia walio katika hatari kutokana na mapigano mjini Juba.

Katika mahojiano na redio ya Umoja wa Mataifa Miraya, nchini Sudan Kusini ,  kaimu msemaji wa UNMISS Shantal Persaud amesema hiyo ni sehemu ya juhudi za kukabliana na ukatili wa kingono na kijinsia.

Amesema UNMISS imeendelea kupokea taarifa ya unyanyasaji wa kingono na kijinsia katika kambi za Umoja wa Mataifa za kuhifadhi wakimbizi na anaeleza hatua zinazochukuliwa.

( SAUTI SHANTAL)

‘‘Kwa sasa idara ya haki za binadamu na msahauri wa ulinzi wa wanawake wameanza kukusanya ushahidi wa vitendo vya uvunjifu wa haki za binadamu,hadi sasa wamesajili zaidi ya visa 100. Ripoti hii ikikamilika, itaepelekwa kwa Katibu Mkuu, ofisi ya kamishana mkuu wa haki za binadamu, na msaidizi wa Katibu Mkuu kuhusu ukatili wa kingono katika maeneo yenye vita.’’

 

♦ Tafadhali iwapo unataka kupokea taarifa kutoka UN News Kiswahili kila wakati zinapochapishwa jisajili  hapa.
♦ Pia unaweza kupakua apu ili kusikiliza matangazo yetu wakati wowote popote ulipo.
♦ Tembelea pia chaneli yetu ya Youtube na pia Soundcloud