Mapigano makali yanaendelea Allepo Syria, wengi wapoteza maisha:UM

Mapigano makali yanaendelea Allepo Syria, wengi wapoteza maisha:UM

Mapigano makali yakihusisha matumizi ya silaha nzito nzito na kuvurumishwa kwa makombora na magrunet yanaendelea mjini Aleppo Syria tangu Jumapili.

Kwa mujibu wa afisa mawasiliano wa shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia watoto UNICEF nchini Syria Kieran Dwyer watu wengi wamepoteza maisha na wengine kujeruhiwa katika mashambulizi hayo huku maelfu wakifungasha virago.

(SAUTI YA DWYER)

"Mapigano makali mahali hapa, watu 25,000 wamekimbia ghafla jana usiku, wakichukua chochote walichoweza kuchukua. Wengine wamo katika bustani, misikitini, wengine wana jamaa zao, na wengine popote pale wanapoweza kuhisi angalau wako salama”