Skip to main content

Changamoto kubwa ni kuendesha mchakato wa uchaguzi kwa wakati Somalia:Keating

Changamoto kubwa ni kuendesha mchakato wa uchaguzi kwa wakati Somalia:Keating

Mwakilishi maalumu wa Umoja wa Mataifa nchini Somalia Michael Keating amesema mchakato wa uchaguzi mkuu wa Somalia unaotarajiwa kuanza mwishoni mwa mwezi huu utakabiliwa na changamoto kubwa ya wakati.

Amesema kuna mambo mengi yanayohijatika kufanyika kabla ya kuanza mchakato huo ili kuhakikisha unakuwa wa kuaminika sio tu machoni pa Wasomali bali pia katika jumuiya ya kimataifa.

Keating amesema jukumu la Umoja wa mataifa katika mchakato huo ni kutoa usaidizi lakini mchakato mzima unaendeshwa na Wasomali wenyewe, na usaidizi wenyewe ni wa kiufundi na ushauri, lakini kikubwa zaidi ni kusaidia wanachokitaka wasomali katika mchakato mzima.