Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Mazingira ya kuwezesha kina mama kunyonyesha popote na wakato wowote yanahitajika:WHO

Mazingira ya kuwezesha kina mama kunyonyesha popote na wakato wowote yanahitajika:WHO

Nchi zaidi ya nchi 170 duniani zinasherehekea wiki ya unyonyeshaji kuanzia leo Agost Mosi hadi Agost 7, ili kuchagiza hulka ya onyonyeshaji kwa nia ya kuboresha afya wa watoto kote duniani.

Kwa mujibiu wa shirika la afya duniani WHO kunyonesha ni njia bora ya kuwapatia watoto wachanga virutubisho wanavyohitaji mwilini, na shirika hilo linapendekeza watoto kupewa maziwa ya mama tuu kuanzia saa moja baada ya mtoto kuzaliwa hadi miezi sita.

Hata hivyo WHO inasema hulka hiyo inatofautina kimataifa mfano ni asilimi 29 tu ya watoto wa chini ya miezi sita ndio wanaonyonyeshwa mazima ya mama pekee kwenye ukanda wa Mediterranean , ikiwa ni chini ya lengo la kimataifa la WHO la kufikia asilimi 50 ifikapo 2013.

WHO inasisitiza kwamba unyonyeshaji unahitaji kulindwa, kuchagizwa na kuungwa mkono , hususani miongoni mwa masikini na makundi yasiyojiweza , il. Lakini pia mazingira bora ya kuhakikisha kina mama wanaweza kunyonyesha popote na waklati wowote yanahitajika.