Baraza la usalama yapitisha azimio la kupeleka polisi Burundi

Baraza la usalama yapitisha azimio la kupeleka polisi Burundi

Baraza la usalama la Umoja wa Mataifa limepitisha azimio namba 2303 la kuepeleka maafisa wa polisi 228 nchini Burundi, taifa ambalo limeingia katika machafuko baada ya uchaguzi mkuu mwaka jana. Maafisa hao ambao watapelekwa nchini humo kwa kipndi cha awali cha mwaka mmoja , watakuwa wakifuatilia hali ya usalama, kusaidia ofisi ya haki za binadamu ya Umoja wa Mataifa katika ufuatilaiji wa ukwepaji wa haki za kibinadamu na vitendo vya ukatili.

Azimio hilo limepitishwa kwa kura 11 huku kura nyingine nne zikiwa hazijachagua upande wowote. Kufuatia kupitishwa kwa azimio hio, baraza la usalama litamwomba Katibu Mkuu kuwasilisha ripoti ya hali ya Burundi kila baada ya miezi mitatu ikiwamo matukio ya machafuko pamoja na kuhakikisha upelekwaji wa polisi wa UM nchini humo.

Akihutubia baraza hilo baada ya kupitishwa kwa azimio hilo, mwakilishi wa kudumu wa Ufaransa katika ofisi za Umoja wa Mataifa François Delattre kupitia mtafsiri anasema.

(SAUTI DELATTRE)

‘Burundi imeshuhudia majanga makubwa miaka iliyopita ambapo ukabila umetika vibaya. Baraza la usalama linachukua jukumu lake leo kuhakikisha kuwa histioria haijirudii. Tunaelewa katika baraza umuhimu wa kuepusha machafuko na hiki ndicho tumekifnay leo kwa kupitisha azimio namba 2303.’’