Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

UNODC yasikitishwa na mauaji Indonesia kuhusiana na dawa za kulevya

UNODC yasikitishwa na mauaji Indonesia kuhusiana na dawa za kulevya

Ofisi ya Umoja wa Mataifa kuhusu dawa za kulevya na uhalifu (UNODC), imeeleza kusikitishwa kwamba Indonesia ilipuuza wito wa Katibu Mkuu kwamba isinyonge baadhi ya wafungwa kwa madai ya uhalifu unaohusiana na dawa za kulevya.

Kama shirika la Umoja wa Mataifa linaloshughulikia tatizo la dawa za kulevya duniani, UNODC imesisitiza kuwa hukumu ya kifo haiungwi mkono na mikataba ya kimataifa ya kudhibiti dawa za kulevya.

Ikimnukuu Katibu Mkuu, taarifa ya UNODC imesema Umoja wa Mataifa unapinga hukumu ya kifo katika mazingira yote, ikiongeza kuwa iwapo iatatumika, hukumu ya kifo inapaswa tu kutumiwa pale unapotendwa uhalifu mbaya zaidi, hususan unaohusu kuua kwa kukusudia, na kwamba uhalifu wa dawa za kulevya hautimizi kigezo hicho.