Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Homa ya ini bado ni changamoto Uganda

Homa ya ini bado ni changamoto Uganda

Tarehe ishirini na nane Julai kila mwaka dunia huadhimisha siku ya homa ya ini. Shirika la afya ulimwenguni WHO huitumia siku hiyo kuhamasisha makabiliano dhidi ya ugonjwa huo hatari.

Katika maadhimisho ya mwaka huu, WHO inazitaka nchi wanachama kuchukua hatua haraka kuboresha ufahamu kuhusu homa ya ini, kuongeza fursa ya kufanyiwa vipimo na kupata huduma ya tiba.

Duniani kote watu milioni 40 wameambukizwa homa ya ini aina B na C, ikiwa ni mara 10 zaidi ya watu wanaoishi na VVU.

Nchi zinazoendelea ni miongoni mwa maeneo ambayo WHO inasema yanashambuliwa vikali na gonjwa hilo. Uduni wa huduma za kupima, kinga na tiba ni sababu ya homa ya ini kutamalaki zaidi katika nchi zenye kipato kidogo.

Uganda ni miongoni mwa nchi hizo za kipacho cha chini . Je mwenendo wa homa ya ini aina ya B pamoja na C ukoje? Tuungane na John Kibego