Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

CAT yaipa Burundi saa 48 kuwasilisha utetezi

CAT yaipa Burundi saa 48 kuwasilisha utetezi

[caption id="attachment_291032" align="alignleft" width="300"]barazaburundi

Kamati ya Umoja wa Mataifa dhidi ya utesaji CAT imeupa ujumbe wa Burundi saa 48 ikiwa ni utaratibu wa kawaida ili kuwasilisha maelezo zaidi, ya majibu kufuatia maswali waliyoulizwa jana na kamati hiyo.

Awali , ujumbe wa Burundi ambao ulipaswa kujibu maswali mbele ya kamati dhidi ya utesaji CAT hii leo mjini Geneva Uswisi, kuhusu hali ya haki za binadamu nchini humo, haukutokea ingawa uliwasilisha barua.

Kamati hiyo katika taarifa yake imesema kuwa ikiwa ujumbe wa Burundi hautojitokeza, watafanya majumuisho kutokana na taarifa walizonazo hadi sasa.

Kuanzia jana kamati ya Umoja wa Mataifa dhidi ya utesaji, CAT ilikuwa ikitathimini hali ya haki za binadamu nchni Burundi kufuatia taarifa za kuzorota kwa haki hizo tangu taifa hilo liingie katika machafuko.

Ubalozi wa Burundi katika ofisi za Umoja wa Mataifa Geneva ulituma barua iliyosomwa na kamati, ambapo umesema kuwa mada zilizobuliwa, hazikugusia mada tano ambazo ziliwasilishwa kwa serikali , kinyume chake yalikuwemo masuala mengine ambayo hayakuwahi kuwasilishwakwenye serikali ya Burundi.