Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Watoto wachanga milioni 77 hawanyonyeshwi katika saa ya kwanza ya uhai wao:UNICEF

Watoto wachanga milioni 77 hawanyonyeshwi katika saa ya kwanza ya uhai wao:UNICEF

Watoto wachanga milioni 77 million  au mtoto 1 kati ya 2 hawanyonyeshwi katika saa ya kwanza baada ya kuzaliwa , na kuwanyima virutubisho muhimu , kinga na uhuisiano wa mwili kwa mwili na mama yake vitu ambavyo vinamlinda mtoto huyo na maradhi na kifo. Joseph Msami na taarifa kamili

(TAARIFA YA MSAMI)

Hayo yamesemwa na shirika la Umoja wa mataifa la kuhudumia watoto UNICEF katika kuelekea wiki ya unyonyeshaji, likisistiza kuwa , kuwafanya watoto wasubiri muda mrefu kuwa karibu na mama zao baada ya kuzaliwa kunapunguza fursa ya kuishi, kunasababisha utokaji wa maziwa kuwa mdogo na watu kutonyonyesha maziwa ya mama tu kwa watoto wao.

Na kuwachelewesha watoto kwa saa 24 au zaidi kunaongeza hatari ya asilimia 80 kwa watoto hao, lakini endapo watanyonyeshwa maziwa ya tu kwa miezi sita ya kwanza basi maisha ya watoto laki nane yataokolewa kila siku.