Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Ujumbe wa Burundi washindwa kujitiokeza mbele ya kamati ya utesaji Geneva

Ujumbe wa Burundi washindwa kujitiokeza mbele ya kamati ya utesaji Geneva

Katika hali isiyokuwa ya kawaida,  ujumbe wa Burundi ambao ulipaswa kujibu maswali mbele ya kamati dhidi ya utesaji CAT hii leo mjini Geneva Uswisi, kuhusu hali ya haki za binadamu nchini humo, haukutokea. Flora Nducha na ripoti kamili.

( TAARIFA YA FLORA)

Kuanzia jana kamati ya Umoja wa Mataifa dhidi ya utesaji,  CAT ilikuwa ikitathimini hali ya haki za binadamu nchni Burundi kufuatia taarifa za kuzorota kwa haki  hizo tangu taifa hilo liingie katika machafuko. Miongoni mwa mambo jadiiwa ni maji ya kiholelea na utesaji hususani kwa viongozi wa upinzani.

Ujumbe huo ulipaswa kujibu maswali ambayo kamati iliyauliza jana  lakini hadi tunakuletea taarifa hizi hakukuwa na mjumbe yoyote aliyewasili kwenye kamati badala yake ubalozi wa ya nchi hiyo kwenye ofisi za UM Geneva,  wametuma barua iliyosomwa kwenye kamati.

Katibu wa CAT Patrice Gillibert, ameuambia mkutano huo kuwa kile kilichoandikwa kwenye barua hiyo.

( SAUTI PATRICE)

’Ujumbe wa Burundi umebaini kuwa mada zilizobuliwa, hazikugusia mada tano ambazo ziliwasilishwa kwa serikali , kinyume chake yalikuwemo masuala mengine ambayo hayakuwahi kuwasilishwa kwenye serikali ya Burundi.’’