Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Homa ya manjano Angola na DRC: zaidi ya visa 5000 na vifo 400 vyashukiwa

Homa ya manjano Angola na DRC: zaidi ya visa 5000 na vifo 400 vyashukiwa

Shirika la Afya Duniani (WHO), limesema kuwa kufikia tarehe 21 Julai 2016, zaidi vifo 400 vilikuwa vimeripotiwa nchini Angola na Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC), karibu nusu vikithibitishwa kutokana na homa ya manjano.

WHO imesema kuwa idadi ya watu wanaoshukiwa kuambukizwa homa hiyo katika nchi za Angola na DRC, imeripotiwa kuwa zaidi ya 3,700, ambapo visa 879 vimethibitishwa.

Kampeni za utoaji chanjo zimeanza katika nchi hizo, hususan katika maeneo yaliyoathiriwa.

Fadella Chaib ni msemaji wa WHO, Geneva..

Kampeni ya chanjo ya halaiki ilianza kwanza Luanda wiki chache zilizopita, na sasa imeenezwa na kufikia maeneo mengine ya Angola yaliyoathiriwa. Karibuni kampeni hizo zimejikita zaidi kwenye maeneo ya mpakani, na pia tunaendelea na kampeni za chanjo kwa kila nyumba, na utoaji chanjo ya kawaida.”