Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Sitisheni uhasama, muenzi mashindano ya Olimpiki: Ban

Sitisheni uhasama, muenzi mashindano ya Olimpiki: Ban

Kuelekea michuano ya olimpiki inayoanzaAgosti tano mjini Rio de Janeiro nchini Brazil, Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-moon ametaka usitishwaji wa uhasama ikiwa ni sehemu ya kuenzi michuano hiyo ya kimataifa.

Katika ujumbe wake Ban amesema michuano hiyo ina hamasa ya kuzishinda changamoto za dunia hususani kwa mambao yaliyoonekana hayawezekani na akataka juhudi ziwekezwe katika kushinda medali uwanjani na kunyamazisha mitutu ya bunduki katika maeneo ya vita.

Amesema kipindi hicho cha kusitisha uhasama kitadhihirisha thamani ya kile kinachotafutwa na olimpiki ambacho ni heshima, urafiki, mshikamano na usawa na kuongeza kuwa tayari mwaka huu michuano ya olimpiki imeweka historia ya kufanyika kwa mara ya kwanza Amerika Kusini pamoja na kujumuisha wakimbizi kama sehemu ya timu.

Ban amesema hatua hiyo ni muhimu kwani itaonyesha uthabiti wa wakimbizi na kuikumbusha dunia kchukau hatua zaidi katika kutatua vyanzo vya madhila yao ambavyo ni machafuko