Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Hukumu dhidi ya wapinzani 30 Gambia yaisikitisha ofisi ya haki za binadamu

Hukumu dhidi ya wapinzani 30 Gambia yaisikitisha ofisi ya haki za binadamu

Ofisi ya Haki za Binadamu ya Umoja wa Mataifa imesema inatiwa hofu na kuhuku ya miaka mitatu jela waliyopewa wajumbe wa 30 wa chama kikuu cha upinzani nchini Gambia ikiwemo kiongozi wao Ousainou Darboe.

Hukumu hiyo iliyotolewa juma lililopita inatokana na kushiriki kwao maandamano ya amani yaliyofanyika katikati mwa mwezi Aprili.

Kwa mujibu wa Rupert Colville msemaji wa ofisi ya haki za binadamu pia..

(SAUTI YA RUPERT COLVILLE)

"Tunatiwa wasiwasi kwamba hakuna uchunguzi wowote wa kina uliofanywa kufuatia madai ya matumizi ya nguvu kupita kiasi dhidi ya waandamanaji, kukamatwa na kufa akiwa kizuizini katibu wa zamani wa chama hiyo cha upinzani.”