Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Taasisi za umoja na uwajibikaji ni muhimu katika ujenzi wa amani:Ban

Taasisi za umoja na uwajibikaji ni muhimu katika ujenzi wa amani:Ban

Taasisi zinazojumuisha wote na za uwajibikaji ni msingi ambao unaunganisha serikali na raia kwa pamoja na ni lazima waimarike.

Hayo ni kwa mujibu wa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-moon akizungumza kwenye baraza la usalama Alhamisi wakati wa mjadala wa wazi kuhusu ujenzi wa amani barani Afrika.

Amesema amani Afrika inasalia kuwa ni kipaumbele cha juu na ameonya kwamba wakati taasisi zikidhoofika nchi haziwezi kushamiri.Ban ameongeza kuwa ujenzi na uimarishaji wa taasisi ni muhimu sana

(SAUTI YA BAN)

"taaisi zinazojumuisha wote na za uwajibikaji ni sementi inayounganisha serikali na raia. Zinatoa usalama, haki, kubana ufisadi, kupunguza utengwaji, na kuepusha mivutano ya kikabila. Kujenga taasisi imara na zinazofanya kazi sio rahisi, lakini tumejifunza somo la msingi, hakuna suluhisho moja kwa kila kitu”