Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Michezo ni jukwaa muhimu katika kutekeleza SDGs: Alhendawi

Michezo ni jukwaa muhimu katika kutekeleza SDGs: Alhendawi

Nats!

Video inayoonyesha umoja na mshikamano katika kambi mbalimbali za timu ya kandanda, Inter Millan ya Italia katika tukio maalum kuhusu nguvu ya kandanda katika kubadilisha dunia ikijikita zaidi katika utekelezaji wa malengo ya maendeleo endelevu SDGs.

Tukio hilo ambalo limeandaliwa na ubalozi wa Italia katika Umoja wa Mataifa limewaleta pamoja wadau mbalimbali wa soka wakiwamo viongozi wa Inter Millan ambao wamejumuika kuelezea namna gani michezo inavyoweza kuhamasisha utekelezaji wa SDGs.

Kwa upande wake mwakilishi maalumu wa Katibu Mkuu kuhusu masuala ya vijana Ahmad Alhendawi ameuambia mkutano huo kuwa vijana, michezo na maendeleo ni kiungo muhimu katika kusongesha juhusi za ajira na utekelezaji wa SDGs.

Amesema vijana wana shauku kubwa kuhusu michezo kuliko mikutano kwa hiyo.

(SAUTI AHMAD)

‘‘Masuala haya sio ya watu wengine, ni ya kila mmoja. Hesabu ni rahisi sana, tuna malengo 17 tunayopaswa kuyatimiiza kwa maiak 15. Tuna malengo mengi kuliko miaka, kwahiyo hatuna muda wa kupoteza.’’