Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Vipimo na majibu ya haraka husaidia kupambana na homa ya manjano:WHO

Vipimo na majibu ya haraka husaidia kupambana na homa ya manjano:WHO

Vipimo vya kuaminika na kupata majibu wakati muafaka ni muhimu katika kufanya maamuzi kuhusu kila pembe ya huduma za afya hususani wakati wa magonjwa ya mlipuko. Hayo ni kwa mujibu wa shirika la afya ulimwenguni WHO, ambalo linasema kufanya vipimo vya homa ya manjano ni changamoto kubwa nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo DRC.

Limesema mara nyingi kuna ucheleweshaji kati ya kukusanywa kwa sampuli na kusafirishwa kwenda kuchunguzwa hadi wakati vipimo hivyo vinapofanyiwa tathimini

Kwa kulitambua hilo na kutaka kuimarisha kuharakisha upimaji, WHO imesaidia kupeleka maabara za kwenye magari , kutoka Muungano wa Ulaya hadi Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo.

Maabara hizo zimewasili na vifaa na dawa zinazohitajika kwa ajili ya kufanya vipimo vya sampuli za damu kwa ajili ya kubaini homa ya manjano. Na maabaraza hizo ni rasihi kufungwa mahali popote palipo na kituo cha afya na kuweza kusaidia maelfu ya watu.