Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Siku ya kimataifa ya homa ya ini, elimu zaidi yahitajika: WHO

Siku ya kimataifa ya homa ya ini, elimu zaidi yahitajika: WHO

Ikiwa leo ni siku ya kimataifa ya homa ya ini yenye  kauli mbiu kutokomeza, shirika la afya ulimweguni WHO limezitaka nchi wanachama kuchukua hatua haraka kuboresha ufahamu kuhusu homa ya ini, kuongeza fursa ya kufanyiwa vipimo na kupata huduma ya tiba.

Duniani kote watu milioni 40 wameambukizwa homa ya ini aina B na C, ikiwa ni mara 10 zaidi ya watu wanaoishi na VVU.

Nchini Tanzania ugonjwa huu haufahamiki kwa kiwango toshelevu. Dk Angelina Sijaona ni mratibu wa homa ya ini katika wizara afya nchini humo.

(SAUTI DK ANGELINA)

Pia ameeleza malengo katika kuhakikisha gonjwa hilo linatokomezwa.

( SAUTI DK ANGELINA)