Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Kamati ya UM dhidi ya utesaji yaitathimini Burundi

Kamati ya UM dhidi ya utesaji yaitathimini Burundi

Kamati ya Umoja wa Mataifa dhidi ya utesaji imekutana Geneva na leo Alhamisi Julai 28 na Ijumaa Julai 29 ikijadili na kutathimini ripoti kuhusu Burundi. Flora Nducha na taarifa kamili.

(TAARIFA YA FLORA)

Kwa mujibu wa kamati hiyo tathimini maalumu inafanyika kufuatia taarifa zilizopokelewa hivi katribuni za kuendelea kuzorota kwa hali ya haki za binadamu nchini humo.

Kamati imesema ripoti maalumu kuhusu ukiukaji wa haki za binadamu Burundi iliitaka serikali hiyo kutanabaisha hatua izilochukua kufanya uchunguzi wa kina kuhusu mauaji ya kiholela, yakiwemo ya kisiasa, utesaji hasa wa wafuasi na viongozi wa upinzani, waandishi wa habari , wanaharakati wa haki za binadamu na mtu yeyete anayeonekana kuunga mkono upinzani. Pia kuchunguza mauaji mengine yote yaliyoripotiwa kuhusuiana na siasa na suala la wa Hivi sasa kamati inasema imeshapokea ripoti ya Burundi . Mwenyekiti wa kamati hiyo ni Saimon Walker

(SAUTI YA WALKER)

“Kamati imepokea ripoti maalumu tarehe 30 Juni 16 na inatathiminiwa leo, napenda kushuru tena kwa serikali kuwasilisha ripoti kutoka kwa serikali ya Burundi na kwa kuwepo hapa leo kwa ajili ya majadiliano, kuhusu hali ya Burundi”