Vifo kutokana na joto kali huenda vikaongezeka- UNISDR

28 Julai 2016

Ofisi ya Umoja wa Mataifa inayohusika na kupunguza athari za majanga (UNISDR), imeonya leo kuwa huenda idadi ya watu wanaofariki kutokana na mawimbi ya joto kali ikaongezeka.

Hii ni kufuatia kiwango cha joto Kuwait kufikia nyuzi joto 54 kwenye vipimo vya selsiasi wiki iliyopita, kikidhihirisha jinsi joto linavyopanda duniani kutokana na mabadiliko ya tabianchi.

Mwakilishi maalum wa Katibu Mkuu kuhusu kupunguza athari za majanga, Robert Glasser, amesema mamilioni ya watu duniani wanapaswa kutahadharishwa kuhusu mawimbi ya joto, ili kuepuka maelfu ya vifo vilivyotokana na mawimbi ya joto mwaka jana, hususan barani Asia na Ulaya.

Amesema juhudi za kudhibiti hatari ya majanga zinapaswa kumulika zaidi hali ya joto kali, ili kupunguza vifo vitokanavyo na janga hilo, hasa katika mwaka huu ambao umo mbioni kuweka rekodi ya kuwa wenye joto kali zaidi.

 

♦ Kupata takwimu za waathirika vitani Ukraine bofya  hapa.
♦ Iwapo ungependa kupokea taarifa kutoka UN News Kiswahili kila wakati zinapochapishwa jisajili  hapa.
♦ Pia unaweza kupakua apu ili kusikiliza matangazo yetu wakati wowote popote ulipo.
♦ Tembelea pia chaneli yetu ya Youtube na pia Soundcloud na Twitter