Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Malawi inahitaji msaada wa zaidi ya chakula: Kang

Malawi inahitaji msaada wa zaidi ya chakula: Kang

Msaidizi wa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa kwa maswala ya Kibinadamu amesema Malawi kama yalivyo mataifa mengine yaliyokumbwa na ukame inahitaji misaada mbali na chakula kwani masuala kama afya, maji na huduma za kujisafi, ulinzi na elimu yanahitajika nchini humo.

Akiongea na waandishi wa habari mjini New York, Bi Kang ambaye alikuwa anaelezea tathimini ya zira yake nchini Malawi amesema, takribani asilimia 40 ya watu ambayo ni zaidi ya watu milioni sita wanakadiriwa kuwa na njaa na ukosefu wa fedha za kununua mahitaji ya msingi.

Bi Kang amesema kuwa ziara hiyo imemkutanisha na akina mama na watoto waliotahiriwa na utapiamlo na kuzungumzia msaada wanaopata, pamoja na jamii zinazopokea msaada wa kuimarisha uzalishaji wa kilimo.

Amesema kilimchomfariji ni.

( SAUTI KANG)

‘‘Licha ya changamoto, nimefurahi kuona jamii zinashiriki katika miradi inatayowasaidia kuinua ustawi wao na kujenga uwezo wa kukabiliana na madhara katika majanga yanayoweza kutokea.’’

Msaidizi huyo wa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa kwa maswala ya Kibinadamu ambaye pia ametembelea Madagascar amesema ukame umeathiri kwa kiwango kikubwa taifa hilo na kwamba usaidizi unahitajika ili kukwamua jamii za nchi hiyo.