Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Mcgoldrick atoa wito wa kusitisha uhasama kwa ajili ya masuala ya kibinadamu Taizz:

Mcgoldrick atoa wito wa kusitisha uhasama kwa ajili ya masuala ya kibinadamu Taizz:

Mratibu wa Umoja wa Mataifa wa Masuala ya Kibinadamu nchini Yemen Jamie McGoldrick ametoa wito wa kusitisha haraka uhasama kwa ajili ya kunusuru masuala ya kibinadamu kwenye jimbo la Taizz.

Amesema anatiwa hofu na taarifa za kuongezeka kwa mvutano kwenye jimbo hilo na hususani kutaka kufungwa kwa mji huo  kuendelea kwa machafuko kwenye mji wa Al-sarari.

Bwana McGoldrick amezikumbusha pande zote kuhusu wajibu wao chini ya sheria za kimataifa wa kuruhusu bila masharti yoyote fursa ya kuwafikia na kutoa huduma za kibinadamu kwa watu wote wanaohitaji msaada. Akaongeza..

(SAUTI YA McGOLDRICK)

“Niko Ebb hivi sasa na kwa bahati mbaya kuna maeneo mengine hayafikiki kutokana na hali halisi, na tumekuwa na majadiliano marefu na pande husika ili kuwe na fursa ya huduma za kibinadamu na tumekuwa na muafaka wa muda ili tuanze kushughulikia masuala kwa kupeleka timu kugawa dawa na msaada mwingine katika maeneo yaliyoathirika ,, hivyo tuko katika majadiliano na pande zote na tutaona nini kitatokea”