Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Baraza la Usalama lakutana kuhusu hali ukanda wa Ziwa Chad

Baraza la Usalama lakutana kuhusu hali ukanda wa Ziwa Chad

Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa, leo limekutana kuhusu hali katika ukanda wa Ziwa Chad, likihutubiwa na Msaidizi wa Katibu Mkuu kuhusu masuala ya kisiasa, Jeffrey Feltman, na Mratibu Mkuu wa masuala ya Kibinadamu, Stephen O’Brien. Taarifa kamili na Amina Hassan.

(Taarifa ya Amina)

Katika mkutano huo, Bwana Feltman na Bwana O’Brien wamezungumza kuhusu hali ya kibinadamu, ulinzi wa raia, na usalama katika ukanda wa Ziwa Chad.

Bwana O’Brien amesema watu katika ukanda huo wanahitaji usaidizi kwa dharura, na kwamba mahitaji ya kibinadamu sasa hivi yamezidi uwezo wa kitaifa na kimataifa kuyakidhi.

Naye Bwana Feltman ambaye amerejea kutoka ziara yake katika nchi za ukanda huo, amesifu nchi za ukanda wa Ziwa Chad kwa juhudi zao katika kupambana na Boko Haram, lakini akasema zinapata shinikizo.

Sauti ya Feltman

“Kufikia sasa, nchi za ukanda wa Ziwa Chad zimeubeba mzigo wa kufadhili mapambano na Boko Haram, licha ya mizozo yao ya kiuchumi. Zimelazimika kuhamisha matumizi ya fedha za umma kutoka kwa huduma za msingi, na kuziweka kwa usalama. Natoa wito kwa jamii ya kimataifa isaidie operesheni za pamoja za nchi hizo, kwa kuchagiza usaidizi unaohitajika kisiasa, kivifaa na kifedha.”