Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Mzungumzo ya Syria kufanyika miwshoni mwa mwezi Agosti :de Mistura

Mzungumzo ya Syria kufanyika miwshoni mwa mwezi Agosti :de Mistura

Matumaini ya mazungumzo ya amani ya Syria yaliyopangwa kufanyika mwishoni mwa mwezi ujao yameanza kuonekana baada ya mkutano wa ngazi ya juu baina ya wawakilishi wa Urusi, Marekani na Umoja wa Mataifa mjini Geneva, Uswisi Jumanne ya leo.

Akizungumza na waandishi wa habari baada ya mkutano huo, mjumbe maalum wa Umoja wa Mataifa kwa ajili ya Syria Staffan de Mistura amewaambia waandishi wa habari kuwa lengo ni kufanikisha mazungumzo ya awamu ya tatu na hivyo pamoja na mambo mengine ulijikita katika usitishwaji wa uhasama.

Amesema ufikishwaji wa misaada, vita dhidi ya ugaidi na mpito wa kisiasa ni miongoni mwa yaliyojadiliwa.

Amesema mkutano huo umefanyika sambamba na ule wa mawaziri wa mambo ya kigeni wa Urusi na Marekani na kwamba kuendelea mbele kwa majadiliano ya amani Syria kunategemea kile walichoafikiana.

( SAUTI DE MISTURA)

‘‘Lengo letu, na nalisema wazi kabisa, ni kuendelea na awamu ya tatu ya majaidiliano ya Syria mwishoni mwa mwezi Agosti . Wakati huo huo, natumaini kwamba hatua ya maelewano kati ya mawaziri wa nchi za nje wa Urusi na Marekani, yatadhihirika na kutengeneza mazingira mujarabu nchini Syria na katika majadiliano ya amani ya Syria.’’