Skip to main content

Mabadiliko ya Makamu wa Rais Sudan Kusini yachochee usitishwaji mapigano: UM

Mabadiliko ya Makamu wa Rais Sudan Kusini yachochee usitishwaji mapigano: UM

Makamu mpya wa Rais wa Sudan Kusini Taban Deng Gai akiwa ameshaapishwa kuchukua nafasi ya Riek Machar, Umoja wa Mataifa umetaka hatua hiyo iwe chachu ya kusitisha mapigano na kurejesha amani katika taifa hilo changa zaidi duniani.

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-moon, kupitia msemaji wake Farhan Haq amesisitiza mjini New York wakati akizungumza na waandishi wa habari kuwa ni muhimu mgawanyiko wowote baina ya vyama ushughulikiwe kwa amani na mjadiliano.

Amesema kile ambacho Umoja wa Mataifa utakifanya hata baada ya mabadiliko hayo ya nafasi ya Makamu wa Rais wa Sudan Kusini.

( SAUTI FARHAN)

‘‘Ujumbe wa Umoja wa Mataifa nchini Sudan Kusini, utaendelea kufanya kazi na serikali ya mpito ya umoja wa kitaifa na wadau wote, katika usaidizi wa utekelezaji wa makubaliano ya amani kwa manufaa ya watu wa Sudan Kusini, kama ulivyopewa mamlaka na baraza la usalama.’’