Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Wahamiaji wa Ethiopia walionusirika katika usafirishaji haramu wa watu warejea nyumbani:IOM

Wahamiaji wa Ethiopia walionusirika katika usafirishaji haramu wa watu warejea nyumbani:IOM

Shirika la Kimataifa la Uhamiaji (IOM), limewasaidia Waethiopia 25 kurejea nyumbani salama baada ya kujikuta wamekwama na kuokolewa nchini  Zambia wakati wakijaribu kwenda Afrika ya Kusini.

Watu hao waliorejea ni miongoni mwa manusura 76 wahamiaji kutoka Ethiopia waliokutwa kwenye kontena ambalo lilikatili maisha ya watu 19  nchini Zambia.

Kwa mujibu wa IOM wahamiaji wote ni wanaume wa kati ya umri wa miaka 18-30 na walikuwa katika safari ya njia ya barabara kwa miezi tisa wakivuka mipaka ya Kenya, Tanzania na Zambia.

IOM imewapa wahamiaji hao msaada wa kurejea nyumbani kwa sababu hawakuwa na njia yoyote ya kuweza kurudi Ethiopia. Msaada huo ni pamoja na usafiri na fedha zitakazowarejesha hadi kwenye majimbo waliyotoka Ethiopia.