Mwakilishi wa UM Somalia alaani shambulizi karibu na uwanja wa ndege

Mwakilishi wa UM Somalia alaani shambulizi karibu na uwanja wa ndege

Mwakilishi maalumu wa Umoja wa mataifa nchini Somalia Michael Keating,  amelaani vikali shambulio la kigaidi leo Jumanne kwenye maeneo ya jirani na uwanja wa ndege wa kimataifa wa Mogadishu ambalo limeua angalau watu kadhaa. Amina Hassan na taarifa kamili.

( TAARIFA YA AMINA)

Washambuliaji wa kujitoa muhanga wamelipua magari mawili yaliyokuwa yamesheheni vilipuzi karibu na uwanja wa ndege . Hakuna mfanyakazi wa Umoja wa mataifa aliyethibitishwa kuuawa.

Al-Shabaab kwa mara nyingine wamefanya shambulizi la kikatili lilolopoteza maisha ya Wasomali amesema Keating. Ameongeza kuwa kuwa Wasomali walio wengi wanapinga njia hizo za kigaidi na kutumia ghasia kufikia malango ya kisiasa.

Keating ametuma salamu za rambirambi kwa familia na marafiki wa waliopoteza maisha na kuwatakia huweni majeruhi.