Skip to main content

Joto la kupindukia Mashariki ya Kati inaweza kuwa ni rekodi mpya ya kikanda:WMO

Joto la kupindukia Mashariki ya Kati inaweza kuwa ni rekodi mpya ya kikanda:WMO

Joto kali la kupindukia ambalo limekuwa likiathri mamilioni ya watu Mashariki ya Kati , linaweza kuwa ni rekodi mpya ya kiwango cha joto ukanda huo wamesema Jumanne wataalamu wa hali ya hewa wa Umoja wa Mataifa.

Tangazo hilo la shirika la utabiri wa hali ya hewa ulimwenguni WMO, limekuja baada vya vipimo nchini Kuwait kufikia nyuzi joto 54 vipimo vya centigrade Alhamisi iliyopita. Kamati maalumu imeundwa kutathimini ushahidi na kuona endapo vipimo hivyo ni vya juu kabisa ukanda wa Mashariki na Asia.

Afisa wa WMO Omar Baddour anasema mabadiliko ya tabia nchi na gesi chafu vimechangia hali hiyo, ingawa inategemea sababu mbalimbali.

(SAUTI YA OMAR BADDOUR)

“Kufikia rekodi hiyo unahitaji kuwa na mchanganyiko wa sababu ikiwemo mzunguko wa hewa, hali ya bahari, msimu na mazingira na mengineyo. Hali hiyo hukutani nayo mara kwa mara”.

Hadi sasa rekodi ya dunia ni nyuzi joto 56.7 vipimo vya centigrade, iliorodheshwa mjini Death Valley, California, mwaka 1913.