Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Marekani yatoa dola milioni 25 kwa UNRWA kusaidia dharura ya mtafaruku wa Syria

Marekani yatoa dola milioni 25 kwa UNRWA kusaidia dharura ya mtafaruku wa Syria

Marekani imetoa mchango wa dola milioni 25 kwa shirika la Umoja wa Mataifa la msaada kwa wakimbizi wa Kipalestina UNRWA, kutokana na ombi la dharura la shirika hilo la kusaidia dharura itokanayo na machafuko ya Syria kwa mwaka 2016.

Fedha hizo zitasaidia operesheni za dharura za UNRWA nchini Syria, Lebanon na Jordan.

Tangazo la msaada huo lilitolewa na waziri wa mambo ya nje wa Marekani John Kerry wakati wa hafla mjini Washington D.C , Julai 12 kama sehemu ya msaada wa Marekani katika masuala ya kibinadamu.

Tangu kuanza kwa vita Syria mwaka 2011 karibu wakimbizi wa Kipalestina 110,000 walioorodheshwa na UNRWA nchini Syria wamelazimika kukimbilia nchi jirani na kwingineko.