Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Ban akaribisha makubaliano ya uhusiano kati ya IOM na UM

Ban akaribisha makubaliano ya uhusiano kati ya IOM na UM

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, Ban Ki-moon, amekaribisha kuridhiwa kwa makubaliano ya uhusiano kati ya Umoja wa Mataifa na Shirika la Kimataifa la Uhamiaji (IOM).

Taarifa ya msemaji wake imesema kuwa baada ya kutiwa saini makubaliano hayo mnamo Septemba 19, 2016, IOM itakuwa shirika linalohusiana na mfumo wa Umoja wa Mataifa.

Aidha, taarifa hiyo imesema kuwa Katibu Mkuu anaamini kuwa kuridhiwa kwa makubaliano hayo na nchi wanachama wa Umoja wa Mataifa na IOM, ni hatua kubwa katika uhusiano wa karibu uliodumu muda mrefu, kati ya IOM na UM.

Ban amesema makubaliano hayo siyo tu yanarasmisha ubia, lakini pia yanaweka ushirikiano wa karibu zaidi kati ya Umoja wa Mataifa na IOM, huku yakihifahiwa mamlaka na wajibu wa mashirika ya Umoja wa Mataifa katika uwanja wa uhamiaji.