Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Ban azungumza na rubani wa ndege ya Solar Impulse

Ban azungumza na rubani wa ndege ya Solar Impulse

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, Ban Ki-moon, amezungumza kwa njia ya video na Rubani Bertrand Piccard, saa tisa kabla ya kutua Abu Dhabi, katika awamu ya mwisho ya safari yake ya kuzunguka dunia kutumia ndege inayotumia nishati ya jua.

Mazungumzo hayo yalirushwa pia moja kwa moja kupitia Facebook, ambapo Ban amemwambia Rubani Piccard kuwa ameruka safari ya kilomita 40,000 bila mafuta, lakini bado ana nyingi.

Akikutana na wanahabari jijini New York, msemaji wa Ban, Farhan Haq, amedokeza kidogo yaliyojiri katika mazungumzo hayo..

“Na amemwambia kuwa Solar Impulse inahitimisha safari yake, lakini safari ya kufikia dunia endelevu, ndiyo sasa inaanza.”